Cannavaro ambaye mkataba wake Yanga unaelekea ukingoni alicheza kwa kiwango cha juu, wakati Yanga ilipocheza na Esparanca wiki iliyopita na kufungwa bao 1-0 mjini Dundo, Angola, hata hivyo Yanga ilisonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.
Nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars alikiri kupokea taarifa kutoka kwa mabosi hao wa Esparanca lakini amedai kuwa mipango yake kwa sasa ni kusaini mkataba mpya Yanga na kama timu hiyo itaamua kumuuza ndipo ataondoka.
“Ni kweli watu wa Esparanca walinifuata na kuonyesha nia ya kunihitaji, nimewapa taarifa zangu zote muhimu na kama watahitaji mazungumzo zaidi ni juu yao.
“Hata hivyo mpango wangu mpaka sasa ni kuongeza mkataba Yanga na muda si mrefu nitasaini miaka miwili, nina malengo makubwa zaidi na Yanga,” alisema Cannavaro.
“Lakini siyo kwamba sitaki kuondoka, naisikiliza Yanga zaidi, kama wataona nafaa kuondoka watasema wenyewe lakini kama watataka nibaki sawa vilevile,” alifafanua Cannavaro.
0 comments:
Post a Comment