Image
Image

Wabunge walia na Upungufu wa sukari unaoonekana kuwa jipu nchini.

Mvutano umeibuka Bungeni kwa wabunge kutaka bunge liahirishe shughuli zake kwa muda ili kuweza kujadili kwa dharura hoja ya upungufu wa Sukari ambayo inalikabili taifa kwa sasa.
Siku chache zilizopita Waziri mkuu Kassim Majali aliwaagiza maafisa biashara wa ngazi za wilaya, mikoa na Taifa kukagua Maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.
Waziri Majaliwa alitoa maagizo hayo 27 Aprili 2016 mjini Dodoma wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya mapato na matumizi ya Ofisi yake na kuliomba Bunge kupitisha,ambapo alikiri kwamba kuna upungufu wa sukari nchini ingawa upo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.
Leo 4 May 2016 akiwasilisha Hoja bungeni Mbunge wa Nzega Mhe.Husein Bashe ambaye alisema hali ya upatikanaji wa sukari kwa sasa ni mbaya na kwamba kunahitajika jitihada za dharura za kutatua hali hiyo hali ambayo ilileta mshike mshike bungeni hapo.
Mara baada ya Bashe kueleza
kuwepo jitihada za dharura kujadili upungufu wa sukari Hata hivyo Naibu Spika wa Bunge Dr.Tulia Ackson Mwansasu alikataa kujadiliwa hoja hiyo kwa kuwa tayari Waziri Mkuu Mhe.Khasim Majaliwa alikwishalieleza bunge kinachofanywa na Serikali kwa sasa kama njia ya kubaini kama upungufu huo wa sukari upo au la.
Wakati wa Hotuba ya Mapato na matumizi ya wizara yake Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa takwimu kutokana kwa wa
taalamu zinaeleza kuwa mpaka hivi sasa zipo tani 37,000 za sukari katika maghala nchini,lakini imekuwa haionekani kwa sababu wafanyabiashara wakubwa wameficha sukari ili waiuze kwa bei kubwa.
"Ninawaagiza maafisa biashara kushughulikia suala hili na kuwachukulia hatua wale wote watakao bainika kuwa wamekwenda kinyume na taratibu tulizojiwekea,"Alisema Majaliwa.
Hata hivyo kwa sasa wachuuzi mb
alimbali wanauza sukari hiyo kwa bei ya juu kuanzia Sh.2,200,2500, mpaka 3000 jambo ambalo linaonekana moja kwa moja bei elekezi zilizotangazwa na Serikali kwamba kilo moja ya Sukari iuzwe shilingi 1,800.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment