Wakati
leo ikiwa ni kilele cha siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani
ambapo kwa Tanzania maadhimisho hayo yanafanyika jijini Mwanza,Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye amewatoa hofu
wanahabari na kuwataka kufichua maovu bila woga wa aina yeyote ili
kuweza kujenga Tanzania ya Pamoja.
Kauli ya Nape inakuja wakati wadau
wa habari sambamba na watu mbalimbali wakipaza sauti zao juu ya
kutooneshwa matangazo ya Bunge LIVE kutoka Dodoma kama
ilivyokuwa ikioneshwa hapo awali jambo lililopelekea hata wanahabari
kutopata nafasi yakurekodi mijadala hiyo kama awali kitu ambacho
kimeonesha sura tofauti ya kuzibwa mdomo kwa kile kinachotakiwa kuripoti
bungeni hapo dodoma.
kuhusu sekeseke hilo Waziri nape wakati wa siku
wa vyombo vya habari jijini Mwanza amesema kuwa kuhusu urushwaji wa
matangazo ya Bunge LIVE bado nafasi ipo nzuri ya kukaa meza moja na wadau hao wa
habari ili kuamua namna bora ya kuboresha suala hilo ili yapatikane
maamuzi ya pamoja ya urushwaji wa Matangazo ya bunge kama ilivyokuwa
mwanzo mwa mabunge yaliyopita.
Amesema pia kufanikisha hili
watazingatia kama serikali kwamba watakapo wasilisha Sheria ya Muswaada wa vyombo
vya habari Bungeni kwaajili ya kujadiliwa watahakikisha kuwa unafuta sheria kandamizi ya
kama ya mwaka 1976, na hivyo kutungwa sheria mpya yenye kuzingatia sera
iliyopo ambayo italingana na maoni ya wadau wa habari juu ya maboresho ya
muswaada huo wa vyombo vya habari.
"Nawahakikishieni kwamba
Tunatunga sheria kwa ajili ya watu Kuna sheria zinalalamikiwa kuwa na
mapungufu Serikali itakaa chini kuangalia namna ya kuzirekebisha!.
Waziri
Nape amewahakikishia wanahabari kwamba kama Serikali watahakikisha kuwa
wanalinda,kutetea,na kuukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari Tanzania.
Aidha
ameongeza kuwa uamuzi wa kuanzishwa studio ya Bunge ni uamuzi
uliopitishwa na Bunge lililopita kabla hata hajawa mbunge hivyo suala
hili nilenye kukaa meza moja na kufikia lengo lenye tija katika sekta
hii ya habari na kila mmoja kupata habari kwa wakati.
Home
News
Slider
Wanahabari watakiwa kufichua maovu bila woga ili kujenga Tanzania mpya na yapamoja.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment