Wanasayansi
kutoka nchini Brazil wanaoendelea kuchunguza ugonjwa wa Zika unaonekana
kuwa ni hatari zaidi tofauti na mwanzo walivyofikiria.
Ugonjwa huo unasababishwa na virusi vya Zika ambavyo vinasababisha kuzaliwa kwa watoto wakiwa na vichwa vidogo.
Wakiongea
na BBC, madaktari hao bingwa wamesema kuwa virusi vya Zika vinaweza
kuwa sababu ya kutokea kwa matatizo ya neva za fahamu kwa mwanamke mmoja
mjamzito kati ya watano wanaoathiriwa na Virusi hivyo.
Mwanzoni
maafisa kutoka CDC waliripoti kuwa virusi vya Zika huenezwa na mbu
lakini njia nyingine ambayo unaweza kuambukizwa ni kufanya mapenzi.
Watafiti wa ugonjwa huo sasa wameanza kukukubali kuwa kuna uhusiano kati
ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na dosari kwenye
ubongo.
Madaktari nchini Brazil wameiambia BBC kuwa asilimia ishirini
ya mimba zilizoathiriwa na ZIKA zitasababisha aina nyingine ya
kuharibiwa kwa ubongo wa mtoto akiwa tumboni.
Watafiti hao wamesema
kuwa asilimia moja ya wanawake walioathiriwa na virusi vya Zika wakati
wa ujauzito kuelezwa kuwa watapata watoto wenye vichwa vidogo.
Bado
watafiti wanaendelea kutafuta chanjo ambayo itasaidia kupunguza kasi ya
ugonjwa huo ambao umeenea zaidi bara la Amerika Kusini.
Home
Afya
Slider
Wanasayansi wakiri kwamba ZIKA sasa ni tishio*wasababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment