Watu 14 wameuawa baada ya waasi wa kundi FDLR kushambulia kijiji kimoja mashariki mwa Congo.
Watu 14 wameuawa baada ya waasi wa kundi FDLR kushambulia kijiji kimoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ripoti kutoka shirika la habari la AFP na jeshi zinasema shambulizi hilo lilifanyika eneo la Miriki, Kilomita 110 (maili 65) kaskazini mwa mji wa Goma.
Viongozi kadhaa wa waasi wa FDLR wamehusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika nchi jirani ya Rwanda.
Kundi hilo la waasi wa Kihutu limedaiwa kuchochea vita vilivyodumu miongo miwili mashariki mwa DR Congo.
0 comments:
Post a Comment