Image
Image

Mahakama yatupiliambali pingamizi la DPP, la utakatishaji fedha linalowakabili Bosi TRA na wenzake Dar es Salaam.

Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupiliambali pingamizi lililowekwa na DPP kupinga kuondolewa shitaka la nane lautakatishaji fedha lililokuwa likiwakabili aliyekuwa kamishna wa TRA Harry Kitilya na wenzake leo 6 Mei 2016.
5 Mei 2016 Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa Mwandamizi Benki ya Stanibic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare walifika katika mahakama kuu kanda ya DSM ili kusikiliza rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha ambapo Upande wa utetezi ulidai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza rufani kwa kuwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu haikumaliza kusikiliza kesi hiyo lakini upande wa serikali ulisema haki wanayo kwa sababu shitaka la nane limeshamalizika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment