Wabunge hao wanawake wamesema kwamba wamekasirishwa na kauli ya Mbunge wa kuchaguliwa kutoka mkoa wa Morogoro Goodluck Mlinga aliyetoa kauli yenye ukakasi ndani ya bunge kwa kusema kwamba.
“Wabunge wa viti maalumu kutoka vyama vya upinzania hawapati nafasi hiyo mpaka wawe na mahusiano na viongozi wa vyama vyao”Alisema Mbunge Mlinga.
Wabunge wa kike wa CUF,CHADEMA, walilazimika kuomba Muongozo kwa Naibu Spika wa Bunge Tulia Acksoni Mwansasu kuhusu suala hilo la kudhalilishwa jambo ambao hakuwasikilizwa ndipo kwa pamoja wakachukua uamuzi wakuonesha kuwa hawajapenda udhalilishwaji huo.
Mara baada ya mvutano huo kwa saa kadhaa Bungeni hapo Naibu Spika Tulia Acksoni aliweza kuamuru askari wa Bunge kuingia ndani na kuwaburuza nje.
Mara baada ya kuburuzwa nje ya ukumbi wa Bunge wabunge hao wanawake wa upinzani walipaza sauti zao kwa kusema kuwa sio jambo la kiungwana kuzuiwa kuhoji udhalilishwaji waliofanyiwa na mbunge huyo wa kuchaguliwa wa Morogoro, Jambo wanaloona kuwa Naibu Spika kawaziba mdomo lakini wao wataendelea mpaka suala hilo liwe na uthibitisho wa kweli dhidi yao.
Wabunge hao sasa wametoka kabisa kwenye viwanja vya Bunge huku msimamo wao ukiwa nikususia vikao vya bunge mpaka pale watakapoitwa na kuombwa radhi kwa kudhalilishwa ambapo pia wameonekana wakielekea kwenda kukutana kwaajili ya kuzungumzia suala hilo ambapo wanatazamiwa watarudi na tamko la pamoja pamoja na mambo mengine mengi.
Kwa upande wake Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja Wanawake CHADEMA, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge wanawake wa Ukawa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kufuatia Mbunge wa viti maalumu Sophia Mwakagenda kuomba mwongozo wa Spika wa Bunge kwa kauli aliyotoa jana Mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga kuzungumza bungeni kuwa wabunge wa CHADEMA ili wapate ubunge wa viti maalumu lazima wawe na mahusiano na viongozi waob amesema kwamba kutokana na suala hilo lazima ifikie hatua kwamba zinakomeshwa kabisa,masuala ya mfumo dume usipite kiasi.
"Kwa sasa tumeafikiana kwamba tunaenda kuandika barua rasmi ya kujitoa kwenye chama cha wabunge wanawake na ijulikane kabisa kwamba kilicho bakia kitakuwa ni chama cha wanawake wabunge CCM" amesema Mdee.
Amesema mpaka kufikia hapo hawana nia ya dhati ya kuendelea na chama hicho cha wanawake kwani kwa kitendo kama hicho ambacho kilikuwa cha kusimama pamoja na kukemea kinaonekana kuegemea upande mmoja tu jambo ambalo halileti picha nzima.
Katika viwanja wa Bunge askari waliovalia yunifomu, Askari wa kutuliza ghasia,Askari kanzu wamezagaa kuhakikisha kuwa wanaimarisha ulinzi ili kusudi kusitokee uvunjifu wa amani baada ya wabunge hao wanawake wa upinzani kutolewa nje.
0 comments:
Post a Comment