Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya walioficha Sukari na kutishia Kuichukua Sukari hiyo na Kuigawa Bure Kwa Wananchi. Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa bei ya juu.
Amesema
wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo
Expire huko Brazili na kuileta nchini ili watengeneze faida na ndo
maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza.
Rais Magufuli ameyasema
hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh, Mkoani Manyara. Rais
ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha kwa usafiri wa gari.
Akiongea
na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais Magufuli
amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari wako
katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili
kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.
Amesema kwa
taarifa alizonazo, kuna mfanyabiashara alienda akanunua sukari pale
Kilombero zaidi ya tani 3000 na hataki kuzichukua hadi leo
Pia amesema kuna mwingine ana godauni huko Mbagala yenye tani 4000 ambazo hataki kuzitoa ili wananchi wakose sukari.
Rais
Magufuli amesema ameviagiza vyombo vya dola viwafuatilie ili
ikithibitika sukari waliificha basi ichukuliwe na kugawiwa bure kwa
wananchi na pia watapigwa marufuku kufanya biashara yoyote hapa nchini.
Home
News
Slider
MAGUFULI:Walioficha Sukari ndani tutaichukua na kugawia wananchi bure na kisha kuwashitaki.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment