Kikao
cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe 29/4/2016, kiliagiza kuwa
yaorodheshwe mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria
wa Manispaa Bw. Burton Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata
hasara, kupoteza Mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.
Kufuatia
makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo, Baraza la Madiwani la
tarehe 4/05/2016, limeamua kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa
Manispaa Bw. Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Richard Chidaga.
Makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo ni:
1. Miradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa, Manispaa vilipaswa kupata shilingi Milioni 900 kwa mwaka kwa uwekezaji huo. Lakini kutokana na mgogoro wa kimkataba Mapato hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi Bilioni 4.5 mpaka sasa.
2.
Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota, Manispaa iliandaa
mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota, hivyo kuwaondoa wapangaji
hao na kubomoa Nyumba hizo longer, wapangaji walifungua shauri la
kupinga kuondolewa katika Nyumba na kutoa madai ya kujengewa nyumba ama
kulipwa fedha za fidia kutokana na Usimamizi hafifu wa shauri hili
Mahakama imeruhusu iliamuru Manispaa kukaa na kumalizana na wapangaji
nje ya mahakama. Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji
kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya mwaka na
kumpatia kila mpangaji kiwanja. Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi
3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo kwa mchanganuo wa shilingi
695,520,000/= pango la mwaka na 2,576,000,000/= fidia ya viwanja 644.
3.Uwekezaji
eneo la Coco Beach Oysterbay Manispaa iliingia mkataba na Q - Consult
Limited, Kampuni hiyo ilishindwa kutekelezwa mradi kwa wakati na
Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-Consult Limited ilifungua shauri ambalo
halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa
ilipoteza kesi hiyo. Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini
haikuwa na hatua zozote zilizochukuliwa na hivyo Manispaa inaweza
kupoteza haki yake. Iliagizwa na Serikali Mwanasheria Mkuu baada ya
tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo
hilo mpaka sasa Mwanasheria alikuwa hajakata rufaa.
4.Mradi wa Ujenzi
wa maduka Makumbusho (Eastern Capital Ltd) Mkataba juu ya uendeshaji wa
stendi haina manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1% ya makusanyo kwa
mwaka sawa na Shilingi Milioni 4 tu kwa mwaka, wakati kabla ya
uwekezaji, local standy Halmashauri ilikuwa ikipata Milioni 12 kwa
mwezi.
5. Kubomolewa kwa ofisi ya Kata ya Msasani, mwananchi
ajulikanaye kwa jina la Chacha aliingilia eneo la ofisi ya kata ya
Msasani na baadae kuishtaki Manispaa. Usimamizi dhaifu wa shauri hilo
kuisababishia mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa
imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna
ufuatiliaji unaendeleaje. Hata hivyo kwa makusudi Bw. Chacha aliamua
kuuza Kiwanda hili kwa Lake Oil CO. Limited wakati shauri
halijaisha.Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa
shauri hilo, yangu upande wa pili ulikataa Jaji, tuna zaidi ya mwaka
hatujapangiwa Jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.
6.
Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment) Hill Road Oysterbay, mradi
inafanyika kwa ubia na mwekezaji Texas Enterprise Company Ltd, mkataba
uliingiwa mwaka 2009, na mradi umesimama kwa muda mrefu sasa.Pamefanyika
mabadiliko katika mkataba na mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini
ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa sababu ya
kuchelewa kwa mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna
makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.
7. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment s) Kiwanda no. 314 Toure Drive.
Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited mkataba uliingiwa 2009.
Mabadiliko
yamefanyika katika Mkataba bila idhini ya Halmashauri na kuisababishia
mradi kuchelewa kukamilika, Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa
kuchelewa kukamilika mradi.
Halmashauri bado inaendelea kufuatilia miradi mwingine ambayo umeingia na haina manufaa kwa Halmashauri.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment