Wauguzi
nchini hii leo wameungana na wauguzi kote duniani kuadhimisha siku ya
waaguzi duniani ambapo katika maeneo mbalimbali nchini kumeelezwa
changamoto zinazoikabili sekta ya afya.
Mkoani Tabora katika
maadhimisho yaliyofanyika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kitete, wauguzi
hao wamesema licha ya changamoto wanazokabiliana nazo, wanajitahidi
kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia maadili ya uuguzi ili kutoa
huduma bora.
Huko Manyara maadhimisho yamefanyika katika Hospitali ya
Haydom iliyoko wilaya ya Mbulu ambapo imeelezwa asilimia 49 ya wanawake
waishio katika kata ya Haydomu wanajifungulia majumbani kutokana na
ukosefu wa vituo vya afya.
Mkoani Mbeya, uongozi wa mkoa huo
umetangaza kuanza kuvipitia vyuo vyote vya uuguzi ambavyo vinatoa
mafunzo ya kada hiyo bila ya usajili, jambo ambalo ni kinyume cha
taratibu, kanuni na sheria za nchi.
Katika mkoa wa Dar Es Salaam,
Mkuu wa mkoa huo Paul Makonda amewataka wauguzi kufanya kazi kwa weledi
na kukwepa matumizi ya lugha chafu kwa wagonjwa.
Amesema pamoja na
wauguzi kukabiliwa na uhaba wa vitendea kazi na mazingira magumu ya kazi
wanatakiwa kuwa wakarimu kwa wagonjwa.
Siku ya wauguzi duniani
huadhimishwa kila mwaka kukumbuka mchango wa mwanzilishi wa huduma za
uuguzi duniani Muuguzi Florence Nightangel aliyejitolea kuhudumia
majeruhi wa vita.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment