Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini - TRA- tawi la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania vimebaini kuwepo kwa bandari bubu 15 .
Bandari hizo zime kuwa zikitumiwa na mtandao wa u halifu unaowahusisha wageni kutoka Kenya kwa kushirikiana na wenyeji kwa ajili ya uingizaji wahamiaji haramu, bidhaa za magendo na dawa za kulevya.
Wakizungumza katika mpaka huo, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji na ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa eneo la Horohoro , MWESIGA LUBALIRA amesema wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu sita ambao wanatumika katika zoezi la kuingiza wenzao nchini kinyume cha sheria kwa kutumia pikipiki maalum kuwasafirisha .
Kuhusu kuwepo kwa bandari bubu zinazotumika kupitisha bidhaa za magendo na kuwahifadhi wahamijai haramu, Afisa wa Kituo cha Forodha tawi la Horohoro , EDWINI IHWATO amesema wamebaini kuwepo kwa bandari hizo na maeneo mengine ambayo wahamiaji haramu wenye asili ya Kisomali wamekuwa wakihifadhiwa wakitokea Kenya , hasa katika maeneo ya Mwakijembe, Daluni na Maili Nane .
Kuf uatia hatua hiyo meneja wa - tra- mkoa wa tanga swalehe byarugaba amesema ingawa jitihada za kukabiliana na matatizo hayo zinafanyika, lakini hali ya uingizwaji wa bidhaa za magendo katika Mkoa wa Tanga upo juu kutokana jiografia ya mkoa hu o.
Home
News
Slider
Bandari bubu 15 zabainika Tanga zikitumiwa na mtandao wa uhalifu unaowahusisha wageni kutoka Kenya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment