Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, MAGESA MULONGO alipokuwa akizungumza na wavuvi wakiwemo wananchi wa vijiji vya Kata ya Bukumi Wilayani Musoma .
Amesema ifikapo Julai mwaka huu Serikali itafunga shughuli za uvuvi katika ziwa hilo kwa kipindi cha miezi mitatu hadi minne kutoa nafasi kwa samaki kuzaliana .
Hata hivyo amewataka wataalam na wadau wa uvuvi , kuisaidia Serikali kutekeleza uamuzi huo bila kuathiri jamii inayoishi kuteg emea shughuli za uvuvi.
Kuhusu suala la uharamia katika Ziwa Victoria na uharifu katika maeneo yote ya nchi kavu, Mkuu huyo wa Mkoa wa Mara amesema Serikali inajipanga kufanya oparesheni kali ambayo itamaliza kabisa matatizo hayo.
0 comments:
Post a Comment