Mke wa Rais, Mama JANETH MAGUFULI amewaomba Watanzania kuwajali wazee na watu wasiojiweza ili jamii hiyo yenye mahitaji maalum ipate kuishi kama watu wengine ikizingatiwa kuwa wazee ni hazina kubwa kwa taifa.
Amesema hayo alipotembelewa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama MARR Y MAJALIWA ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kumueleza shughuli mbalimbali anazojishughulisha nazo ikiwa ni pamoja na kuwajali wazee na watu wenye ulemavu.
Amesema amani iliyopo hapa nchini kwa kiasi kikubwa imechangiwa na wazee , hivyo wakati umef ika kwa Watanzania wenye nafasi mbalimbali kujitokeza kuwasaidia wazee na watu wenye mahitaji maalum ili jamii hiyo nayo ijione haijatengwa na jamii .
Mama MARRY MAJALIWA amemshukuru mke wa Rais kwa kumualika ofisini kwake na kujion ea shughuli anazozifanya katika kusaidia wazee na watu wenye ulemavu hapa nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment