Wawakilishi wa Algeria katika kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa vilabu barani Afrika, Klabu ya Entente Setif wamebanduliwa nje ya mashindano hayo.
Shirikisho la soka barani CAF imeiondoa Entente Setif kufuatia utovu wa nidhamu wa mashabiki wake timu hiyo ilipokuwa ikichuana dhiai ya klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Mechi hiyo ya tarehe 18 Juni ilisimamishwa na muamuzi baada ghasia kuibuka miongoni mwa mashabiki wa timu hizo mbili.
Mechi hiyo iliposimamishwa Sundowns walikuwa wakiongoza mabao 2-0.
Caf inasema kuwa mawe na vitu vingine vilitupwa uwanjani pamoja na fataki na kusababisha mechi hiyo kutibuka.
Baada ya muda mashabiki walivamia uwanja wakipinga matokeo hayo.
Hata hivyo uamuzi huo wa CAF utaidhuru klabu hiyo ya Sundowns, kwani CAF ilifutilia mbali matokeo ya mechi hiyo.
Hiyo inamaanisha kuwa sasa mbali na Setif kutupwa nje ya mashindano Mamelodi Sundowns itapoteza mabao yake mawili na ushindi huo ambao ungeisaidia kusonga mbele katika mashindano hayo ya kifahari.
Timu zingine katika kundi hilo ni Enyimba ya Nigeria na Zamalek ya Misri - ambao sasa wanaongoza kundi hilo .
Entente Setif walitwaa kombe hilo mwaka wa 2014
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment