Waingereza wameamua kujitoa kutoka kwa Umoja wa Ulaya kufuatia kura ya maoni iliyofanyika jana.
Waziri Mkuu wa Uingereza Dvid Cameron ametangaza anajiuzulu kufuatia matokeo hayo akisema hawezi kuiongoza nchi hiyo katika mazingira mapya yaliyojitokeza.
Cameron,ambaye ndiye aliyependekeza kufanyike kura hiyo ya maoni ili Waingereza waamue kubakia au kujiondoa kutoka kwa Umoja wa Ulaya, amesema atang'atuka kabla mwezi Oktoba mwaka huu.
Matokeo yameonyesha kambi iliyotaka Uingereza ijiondoe kutoka kwa Umoja wa Ulaya imepata asilimia 52 ya kura ikilinganishwa na upande uliotaka ibaki ambao umepata asilimia 48.
Watu wanaoishi katika mji London na Scotland ndio waliopiga kura kwa wingi kusalia ndani ya muungano huo.
Wandani wa maswala ya afisi ya waziri mkuu Bwana David Cameron,wanasema kuwa sasa Britain imeingia katika eneo jipya.
Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanahofu athari za kujiondoa kwa Uingereza kwenye muungano huo utabainika katika masoko ya hisa huku kukitarajiwa athari kubwa kiuchumi kisiasa ndani na nje ya bara Ulaya.
Sarafu ya Euro imepanda katika masoko ya fedha huku Paundi ya Uingereza ikiendelea kuporomoka ikiwa ni ishara kuwa wafanyabiashara wanatarajia Uingereza kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya.
Kwa mujibu wa ripoti waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni inaonyesha kuwa wengi.
Hadi sasa ni majimbo machache ndio hayametangaza matokeo yao na inaonyesha mchuano ni mkali kati ya wanaotaka kubakia na wale wanaotaka Uingereza kujiondoa ndani ya Umoja huo wa Ulaya.
Home
Kimataifa
Slider
BreakingNews:Uingereza yajiondoa kutoka kwa Umoja wa Ulaya*Cameron atoa msimamo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment