Kufuatia kufaulu kwa kura ya kujiondoa kutoka kwa muungano wa ulaya viongozi wakuu wa mataifa ya muungano wa Umoja wa Ulaya wamekuwa akielezea masikitiko yao.
Wanasiasa wakuu barani Ulaya na maeneo mengine duniani wameshikwa na mshutuko mkubwa kufuatia hatua hiyo ya Uingereza.
Mkuu wa muungano wa Ulaya Donald Tusk amesema kuwa mataifa yaliyosalia 27 ya EU yataendelea mbele na ushirikiano.
Aidha amesema kuwa mataifa 6 wanachama wakuu wa muungano huo wa Ulaya yatakutana jumamosi kujadili hatma ya muungano huo ambao bado sasa unatishiwa na kujiondoa kwa mataifa mengine ambayo pia yanakabiliwa na shinikizo la kujiondoa.
Wabunge wa upinzani wa Ufaransa Uholanzi na Denmark wanatishia kuitisha kura ya maoni kama iliyoitishwa huko Uingereza.
Rais wa bunge la EU Martin Schulz, ameiambi runinga ya Ujerumani kuwa anaheshimu matokeo ya uamuzi huo wa waingereza, lakini ana jukumu la kulinda muungano wa EU na sarafu ya Euro ya muungano huo.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, anasema kuwa ni huzuni kubwa kwa Uingereza na Bara Ulaya.
Naye Naibu Kansela wa Ujerumani Sigmar Gabriel ameandika kwenye Twitter "damn",.....huku thamani ya sarafu ya Uingereza, ikishuka pakubwa, mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Wafanyibiashara wamepandwa na ghadhabu kubwa kutokana na matokeo ya kura ya maoni nchini Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment