Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendelea WAMA Mama Salma Kikwete amezitaka Taasisi na wadau mbalimbali kuendelea kusaidia wanawake hasa kuwapa elimu ili kujenga Taifa lenye usawa wa kijinsia katika ngazi za kielemu, kisiasa na hata kiuchumi.
Mama Kikwete amesema hayo katika ofisi za Taasisi hiyo zililopo Kawe Jijini Dar es Saalam wakati wa hafla fupi ya kupokea vifaa mbalimbali vya maofisini zikiwemo kompyuta ikiwa ni ahadi aliyeitoa mke wa Rais wa China mwaka juzi wa kusaidia taasisi hiyo ambpo licha ya kupongeza hatua hiyo amesema ipo haja wadau mbalimbali kuendelea kusaidia harakati mbalimbali za wanawake hapa nchini.
Balozi wa China nchini Tanzania akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya mke wa Rais wa China amesema serikali ya china imekuwa na ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi,kisiasa,na hata kijamii ambapo amesema kwa niaba ya serikali hiyo wataendeleza ushirikiano huo ili kuinua uchumi baina ya nchi hizo mbili.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri akiwemo mwenyekiti mtendaji wa makamuni ya ipp dr regnard mengi.
Home
News
Slider
Mama Salma Kikwete amezitaka Taasisi na wadau kusaidia wanawake ili kuweka usawa wa kijinsia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment