Image
Image

Clinton ashinda kura ya mwisho ya mchujo 2016 katika mji mkuu wa Marekani.

Hillary Clinton  amepata ushindi  muhimu  katika  kura ya mchujo  jana  katika  mji mkuu  wa  Marekani, ikiwa  ni  kura ya  mwisho  katika  kura  za  mchujo  kuelekea  uchaguzi wa  rais  kwa  mwaka  huu 2016, wakati  hali  sasa inahamia  katika  mpambano  dhidi  ya  hasimu  wake kutoka  chama  cha  Reupblican  Donald Trump.
Clinton  alishinda  kwa  asilimia  79  dhidi  ya  asilimia  21 alizopata  Bernie Sanders, wakati  ambapo  kura  karibu zote  zimekwisha  hesabiwa.
Huu  ni  mwisho  mbaya  kwa  seneta  Bernie Sanders  wa jimbo  la  Vermont, ambaye  alileta hamasa  nyingi  kwa Waliberali  na  wapiga  kura  huru kwa  kampeni  katika matawi  ambayo  ilileta  changamoto  kubwa  dhidi  ya Clinton.
Clinton  na  Trump  wameshaanza  kutupiana  maneno  na kutoa  misimamo  tofauti  katika  kupambana  na  ugaidi kufuatia  mauaji  katika  klabu  ya  mashoga  mjini Orlando.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment