Image
Image

Cristiano Ronaldo ashindwa kuisaidia timu yake katika michuano ya Kombe la Euro 2016.

NYOTA wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ameshindwa kuisaidia timu yake katika michuano ya Kombe la Euro 2016 na kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya wapinzani wao Iceland.
Iceland hawakupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo mbele ya mastaa wengi wa Ureno, hata hivyo Iceland walikuwa wanacheza mchezo wao wa kwanza wa mashindano makubwa Ulaya.
Ureno walikuwa wa kwanza kupata bao ambalo lilifungwa na mshambuliaji wao Nani, lakini Iceland wakapambana na kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wao, Birkir Bjarnason.
Katika mchezo huo, Ronaldo alionekana mara kwa mara akijaribu kupambana lakini hakufanikiwa kufanya lolote kama ilivyodhaniwa na wapenzi wengi wa soka.
Ronaldo ameingia kwenye mashindano hayo akiwa ametoka kuipa klabu yake ya Real Madrid ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa bao lake la mwisho katika mikwaju ya penalti dhidi ya Atletico Madrid.
Katika mchezo huo, mchezaji wa timu ya Ureno, Renato Sanches, ameweka rekodi ya kucheza huku akiwa na umri mdogo zaidi kwenye timu hiyo katika mashindano makubwa akiwa na miaka 18 na siku 301, wakati huo Cristiano Ronaldo  aliwahi kucheza akiwa na miaka 19 na siku 128.

 Like ukurasa wetu wa Facebook hapo, kwa kuweza kupata taarifa zaidi, kila zinapo tufikia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment