Image
Image

Kerry: Marekani inatekeleza kwa makini makubaliano ya suala la nyuklia ya Iran

Waziri ya mambo ya nje ya Marekani Bw. John Kerry amesema Marekani inatekeleza kwa makini makubaliano yaliyofikiwa na pande mbalimbali kuhusu suala la nyuklia la Iran, na kutaka kampuni na benki za Marekani zishirikiane na pande husika za Iran.
Bw. Kerry amesema akiwa ziarani nchini Norway kuwa kutokana na vikwazo vya miaka mingi, Iran ina kazi nyingi za kufanya ili benki na kampuni za kigeni ziweze kufahamishwa vizuri hali ya sekta husika nchini humo.
Kabla ya kutoa kauli hiyo Bw Kerry alikutana na mwenzake wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif wakizungumzia mambo yanayohusu maendeleo ya utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia, kuondoa vizuizi, na biashara ya benki. Bw. Zarif juzi alisema japo Marekani imetangaza kuondoa vikwazo dhidi ya Iran, lakini bado kuna nia ya kuiwekea vizuizi na ameitaka Marekani itekeleze kivitendo makubaliano yaliyofikiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment