Durtete aapishwa kuwa rais wa 16 wa Ufilipino
Rais
mpya wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameapishwa leo, baada ya kuahidi kuwa
vita kali dhidi ya uhalifu ndiyo kitakuwa kipaumbele cha mhula wake wa
miaka sita. Durtete amekula kiapo mbele ya hadhira ndogo katika ikulu ya
Malacanang, badala ya mkutano wa umma kama walivyofanya watangulizi
wake. Programu yake ya kupambana dhidi ya uhalifu inahusisha mipango ya
kurejesha adhabu ya kifo, amri za kupiga risasi na kuuwa kwa vikosi vya
usalama na kutoa zawadi kwao kwa kuikabidhi miili ya wauzaji wa madawa
ya kulevya. Akijibu hoja za wakosoaji wa mikakati yake ya kupambana na
uhalifu na ufisadi, Duterte amesema: "Nataka niseme hivi: Nimeona namna
rushwa ilivyoikosesha serikali fedha nyingi, zilizokuwa zimepangwa kwa
ajili ya kuwaondoa mamilioni katika hali mbaya ya umaskini waliomo.
Nimeona namna madawa haramu yanavyoharibu watu na kuvunja mahusiano ya
kifamilia." Durtete, mwendesha mashtaka wa zamani mwenye umri wa miaka
71, na meya wa zamani wa mji wa kusini wa Davao, alipata ushindi mkubwa
katika uchaguzi uliyofanyika mwezi Mei, na ameahidi kuwasafisha wahalifu
nchini humo pamoja na wezi ndani ya serikali katika kipindi cha miezi
sita.
0 comments:
Post a Comment