Image
Image

Theresa May atangaza nia kumrithi Cameron.


Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Theresa May amezindua harakati zake za kumrithi waziri mkuu David Cameron, na kuongoza chama cha Wahafidhina, Conservative leo, akiahidi kuheshimu matokeo ya uamuzi wa wapigakura wiki iliyopita, kuiondoa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya. Waziri huyo amesema pia hakupaswi kuitishwa uchaguzi mwingine kabla ya 2020, ambao ndiyo muda wa kumalizika kwa muhula wa bunge la sasa, na pia hakupaswi kuwapo hatua za dharura za kibajeti, kushughulikia mtikisiko unaoweza kuikumba sekta ya ufadhili wa umma, kutokana na mdororo katika uchumi uliosababishwa na matokeo ya kustukiza ya kura ya maoni iliyopewa jina la Brexit. Wengine wenye nia ya kurithi mikoba ya Cameron ni pamoja na meya wa zamani wa London Borisn Johnson na waziri wa sheria Michael Gove.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment