Jamhuri ya Ireland imesema ukombozi wa nchi peke yake hautoshi kama wanawake hawatakuwa huru dhidi ya mifumo ya ukandamizaji kwa kutoshirikishwa ipasavyo katika nyanja za elimu, afya uchumi na nafasi za uongozi.
Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa nchi hiyo hapa nchini Bi FIONNUALA GILSENAN wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya balozi huyo kukutana na wanautamaduni wanawake wa Tanzania na wale wa Ireland kujadili ni jinsi gani mwanamke anaweza kujikomboa na kuwa chachu ya maendeleo.
Majadiliano hayo yalikwenda sanjari na kumbukumbu ya miaka 100 tangu mapinduzi na uhuru wa Ireland ambapo balozi huyo amesema wanawake wamekuwa na mchango mkubwa katika jitihada za kulikombomba taifa hilo.
Kwa upande wao baaadhi ya washiriki wamesema Tanzania imekuwa ikipiga hatua kila siku na wanawake kujikomboa dhidi ya mfume dume katika kujiletea maendeleo yao nay ale ya taifa kupitia ngazi mbalimbali ambazo zimewezesha wanawake kuchukuwa nafasi kubwa ya uongozi hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment