Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa harambee ya uchangishaji fedha za ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro ambayo litagharimu shilingi bilioni 4.5.
Aidha amekea vikali tabia ya wanafunzi wa kike walioko vyuo vikuu kuacha tabia ya kikahaba inayoonekana kukithiri kwa kujihusisha na vitendo vya kuuza miili yao hali inayosababisha kupoteza utu wa mwanamke.
Naye Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa LUGANO KUSILUKA amesema Chuo Kikuu Mzumbe kina historia ya muda mrefu na kutaja viongozi mbali mbali waliosoma chuoni hapo na kwamba ipo haja ya kila mmoja wao kuguswa na uchangiaji huo.
0 comments:
Post a Comment