Image
Image

Jela miaka 30 kwa atakayeoa au kuolewa na mwanafunzi wa shule ya msingi au Sekondari.



SERIKALI imewasilisha bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2016, unaokusudia pamoja na mambo mengine, kutoa adhabu ya miaka 30 jela kwa mtu yeyote atakayeoa au kuolewa na mwanafunzi wa shule ya msingi au ya sekondari.
Adhabu hiyo iko katika marekebisho yanayokusudiwa kufanywa katika Sheria ya Elimu Kifungu cha 60 kinachokusudiwa kufanyiwa marekebisho kwa kuongezewa vifungu vinavyopiga marufuku ndoa kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.
Kifungu cha 60 A kifungu kidogo cha kwanza ambacho ndio kipya kimeeleza kuwa itakuwa kinyume cha sheria katika mazingira yoyote yale kwa mtu yeyote kumuoa au kuolewa na mwanafunzi wa shule ya sekondari au ya msingi.
Kwa mujibu wa kifungu hicho kipya, mtu yeyote atakayekiuka kifungu hicho, sheria hiyo imeweka wazi kuwa atakuwa ametenda kosa na adhabu yake itakuwa kufungwa jela miaka 30.
Sehemu ya tatu ya sheria hiyo imeeleza wazi kuwa mtu yeyote atakayempa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi au wa shule ya sekondari, atakuwa ametenda kosa, ambalo adhabu yake pia ni kwenda jela miaka 30.
Sheria hiyo imekwenda mbali zaidi kwa watu watakaokutwa na hatia ya kushawishi mwanafunzi wa shule ya msingi na shule ya sekondarin aoe au aolewe, wakati akiendelea na shule, naye atakuwa amefanya kosa na adhabu yake ni faini isiyopungua Sh milioni tano, au kwenda jela miaka mitano au vyote kwa pamoja.
Ili kudhibiti hali hiyo, sheria hiyo imewataka wakuu wa shule na walimu wakuu kutunza taarifa na kuziwakilisha kwa kamishna wa serikali au mwakilishi wake itakayoeleza kwa kina matukio ya ndoa na mimba za wanafunzi na hatua zilizochukuliwa za kisheria dhidi ya waliokutwa na hatia.
Marekebisho hayo ya sheria ya elimu, yamewasilishwa bungeni wiki hii, wakati Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) likiitaja Tanzania kuwa moja ya nchi tatu zinazoongoza kwa ndoa za utotoni.
Taarifa ya shirika hilo iliyotolewa mwanzoni mwa mwaka huu, imeeleza kuwa changamoto hiyo ya ndoa za utotoni nchini, husababishwa na mila potofu, elimu duni na umaskini unaosababisha wazazi kuwa na tamaa za kupata mali ili wakidhi haja zao pamoja na sheria kandamizi.
Kwa mujibu wa takwimu za shirika hilo, Tanzania ni nchi ya tatu inayoongoza kwa ndoa za utotoni duniani kwa kuwa na kiwango cha juu cha ndoa hizo. Hata Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mipango akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi na Mpango wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017, alilalamikia tatizo la mimba za utotoni kuwa limeongezeka na linachangia kurudisha nyuma maendeleo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment