Image
Image

KESI YA MWANGOSI:Askari Pasificus apatikana na kesi ya kujibu.

Leo 22 June, Mahakama kuu kanda ya Iringa imemkuta na kesi ya kujibu askari wa jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia FFU mjini Iringa Pasificus Cleophace Simon kutokana na mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel ten Daud Mwangosi.
Hatua hiyo ni baada ya mahakama kusikiliza ushahidi wa tukio hilo ambapo jumla ya mashahidi wanne wametoa ushahidi wao akiwemo aliyekuwa kamanda wa kikosi cha FFU mjini Iringa Said Mnunka, mkuu wa kituo cha polisi mjini Mafinga Ancelin Mwampamba Lewis Teikya wote kutoka jeshi la polisi na Flora Mhelela anayetambulishwa kama mlinzi wa amani.
Jana 21 june Wakili wa up
ande wa utetezi Rwezaula Kaijage aliiambia Mahakama kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi walioletwa na Jamhuri hauoneshi moja kwa moja kuwa mshitakiwa ndiye aliyetenda kosa hilo na badala yake mashahidi hao wanadhania kuwa mshitakiwa huyo ndiye aliyetenda kosa.
Jana pia Wakili wa utetezi aliendelea kufafanua kuwa hata ushahidi uliotolewa na mashahidi watatu kati ya wanne uliegemea kwenye picha iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi toleo la septemba tatu 2012 ambayo hata mpiga picha wa picha hiyo hakuhojiwa mahakamani hapo.
Aidha aliAongeza kuwa ushahidi uliotolewa na mlinzi wa amani ukimnukuu mshitakiwa kukiri kutenda kosa
hilo huko kijijini Nyololo siku ya septemba 2 2012 hauthibitishi mahakama kuwa mshitakiwa ndiye aliyetenda kosa hilo kwakuwa kabla ya kuhojiwa na mlinzi huyo wa amani mshitakiwa aliitwa na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa wa wakati huo na kwamba inawezekena alipewa maelekezo kukiri kosa hilo hivyo upande wa utetezi unaona ushahidi huo haumtii hatiani mshitakiwa na unaiomba mahakama kumwachia huru kwakuwa hana kesi ya kujibu.


Hata hivyo jana Hoja hiyo ilipingwa na mawakili wa upande wa Jamhuri Sunday Hyera na Ladislaus Komanya wakisema kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamhuri ikiwemo picha iliyochapishwa na gazeti la mwananchi toleo la septemba tatu 2012 ukimuonesha mtuhumiwa akiwa amemuelekezea bunduki aina ya long range inayotumika kulipua mabomu ya machozi pamoja na mabomu ya kishindo huku akijua bunduki hiyo hutumika kupiga kwenye digrii 40 hadi 45 jambo linaloonesha mshitakiwa huyo alikusudia kumuua marehemu Mwangosi.
Jaji aliyesikiliza kesi hiyo Mheshimiwa Dokta Paul Kihwelo aliahirisha kesi hiyo hadi leo 22 June  ambapo mahakama imetolea maamuzi kama mshitakiwa anayo kesi ya kujibu au kumwachia huru ambapo imemkuta na kesi ya kujibu askari Pasificus Cleophace Simon.
Taarifa zaidi baada ya muda.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment