Katika kusimamia ubora wa elimu nchini Serikali kupitia Taasisi ya elimu nchini imeanzisha kitengo maalum chini ya idara ya Utafiti wa Habari na machapisho ili kuratibu na kusimamia shughuli za kutathimini vitabu na maandiko ya kutekeleza mitaala ikiwa ni pamoja na vitabu vilivyoandikwa na waandishi binafsi.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Profesa JOYCE NDALICHAKO alipokuwa akijibu swalila mbunge wa Viti Maalum ANGELINA MALEMBEKA aliyeuliza Serikali imeandaa utaratibu gani kudhibiti vitabu visivyo na maadili mema kwa watoto na ina mpango gani wa kuimarisha kitengo cha udhibiti na usimamizi wa vitabu.
Profesa NDALICHAKO amesema Wizara ya elimu kupitia taasisi ya Elimu nchni imeandaa na kutoa muongozo wa kutathamini maandiko ya kutekeleza mitaala ikiwa ni pamoja na vitabu vinavyoandikiwa na kutolewa na wahidani pamoja na kiada vinavyoandaliwa na TET.
Aidha amesema wizara ya elimu, sayansi na teknolojia kupitia taasisi ya elimu nchni imeanzisha somo la urai na maadili kuanzia darasa la tatu hadi sita ili kuwajengea uwezo watoto wa kitanzania wa kuyafahamu ipasavyo maadili na utamaduni wa kitanzania.
Home
News
Slider
Seikali kudhibiti vitabu vinavyochapishwa na waandishi binafsi visivyo na maadili kwa watoto.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment