Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Bigwa hadi Kisaki ili kuwaondolea kero ya usafiri wananchi wa maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, EDWIN NGONYANI amesema hayo aliokuwa a kijibu swali la M bunge wa Morogoro Kusini, PROSPER MBENA aliyeuliza ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza ili wananchi waliowekewa alama kubomolewa nyumba zao waanze maandalizi ya kuhama.
Naibu Waziri amesema serikali imeanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa sehemu ya barabara ya Bigwa hadi Mvu h a yenye urefu wa Kilomita 78 kwa gharama ya Shilingi BILIONI 714.471.
Amesema fidia italipwa moja kwa moja kwa kila mwananchi anayestahili fidia kwa mujibu wa sheria ya barabara namba 13 ya mwaka 2007 na kanuniza mwaka 2009.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment