Bunge limeambiwa kuwa Serikali imeanza mchakato wa kuboresha sheria ya kukusanya kodi ya magari inayoitwa Motor Vihicle au Road Licence ikiwa ni pamoja na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuhudumia wamiliki wa magari ambayo yatakuwa yamesimama kwa kipindi kirefu bila ya kutembea barabarani kwa sababu za msingi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango,Dakta ASHATU KIJAJU alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kusini, DESDERIUS MIPATA aliyetaka kujua Serikali inampango gani wa kuitizama upy a sheria hiyo .
Dakta KIJAJU amesema kuwa sheria hiyo haitoi unafuu wowote kwa gari lililosimama kwa muda mrefu bila ya kutembea barabarani akaongeza kuwa utaratibu huo umekuwa unaleta adha kwa wamiliki wa magari na hasa pale ambapo kuna usha h idi wa kutosha kwamba gari husika limesimama kwa muda mrefu kwa sababu za msingi.
Akaongeza kuwa baada ya taratibu zote kukamilika mapendekezo ya mabadiliko ya sheria hiyo itapelekwa bungeni ili kujadiliwa na k uiidhinishwa na bunge kwa kad iri itakavyoonekana inafaa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment