Image
Image

Kitilya na wenzake ngoma bado nzito Mahakamani.

MAHAKAMA ya Rufani Tanzania imeamuru jalada la kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa rufani ya Jamhuri.
Kadhalika, mahakama hiyo imeagiza jalada hilo lipangiwe jaji mwingine wa kusikiliza rufani hiyo ya kupinga kuondolewa shtaka la utakatishaji fedha katika kesi inayowakabili washitakiwa hao ya kujipatia dola za Marekani milioni 6.
Uamuzi huo ulisomwa jana na Msajili wa Mahakakama ya Rufani, Zahra Maruma, baada ya shauri hilo kusikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na mwenyekiti Salum Masati akisaidiana na Kipenka Musa na Augustine Mwarija kutupilia mbali pingamizi lililokuwa limewekwa na upande wa washitakiwa.
Msajili Maruma alisema mahakama hiyo imeona kwamba Jaji Mfawidhi Moses Mzuna alikosea kukubali pingamizi la utetezi na kutupilia mbali kusikiliza rufani ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya Kitilya na wenzake.
“Mahakama hii imebatilisha uamuzi uliotolewa na Jaji Mzuna na imeamuru jalada lirudishwe Mahakama Kuu kwa ajili ya kupangiwa jaji mwingine wa kusikiliza rufani ya upande wa Jamhuri kuhusu kuondolewa kwa shtaka hilo” alisema na kuongeza:
“Kwa kuondolewa shtaka hilo Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hakuwa na namna ya kurudi Mahakama ya Kisutu kuomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashitaka kwa sababu kila shitaka linajitegemea na la kutakatisha fedha lilishaondolewa katika hati a mashtaka dhidi ya washtakiwa.”
Mapema Mei 31, mwaka huu, upande wa Jamhuri ukiongozwa na DPP, Biswalo Mganga, Naibu DPP, Osward Tibabyekomya, mawakili wa serikali waandamizi, Shadrack Kimaro na Awamu Mbagwa uliomba mahakama hiyo kuangalia uhalali wa kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha pamoja na uamuzi wa Jaji Mzuna kutupilia mbali rufani yao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment