MKAKATI madhubuti umeandaliwa ili kulinda ubora wa pamba ya Tanzania katika soko la dunia pamoja kumnufaisha mkulima wa zao hilo nchini.
Moja ya mkakati huo ni kwa wafanyabiashara wenye tabia ya 'kuchakachua' mizani kwa lengo la kuwaibia wakulima wa pamba watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kushtakiwa mahakamani.
Aidha, wakulima watakaobainika kuongeza vitu visivyofaa kwenye pamba kwa lengo la kuongeza uzito, watakabiliwa na adhabu ili kuifanya pamba ya Tanzania kuwa na ubora zaidi katika soko la dunia.
Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), jijini Dar es Salaam jana, Iren John.
Iren alifafanua kuwa wakati wa msimu wa pamba wafanyabiashara huchezea mizani ili wapate pamba nyingi, hivyo kuzidi kumuumiza mkulima.
Alisema kila ukifika msimu wa pamba, wanunuzi hao hutumia mizani iliyochakachuliwa na kuwaibia wakulima wa zao hilo, jambo ambalo limekuwa likiwaumiza na kuwafanya kuacha kulima zao hilo na kuhamia kulima mazao mengine.
“Kutokana na tabia ya wanunuzi kuchezea mizani, wakulima nao huamua kuongeza vitu visivyofaa kwenye pamba yakiwamo maji, mchanga na hata mawe ili kupata kilo nyingi, matokeo yake pamba ya Tanzania inapofika katika soko la dunia hushushwa bei kwa kukosa ubora," alisema na kuongeza:
"Zamani pamba ya Tanzania iliitwa dhahabu nyeupe kwenye soko la dunia, tulikuwa tukichukua alama ya kwanza kwa ubora wa pamba yetu, hivi sasa hali imebadilika baada ya kuzuka mchezo huo mchafu.
Alifafanua kuwa ili kukabiliana na hali hiyo, WMA imeamua kuzunguka mikoa yote inayolima pamba hususan Kanda ya Ziwa kutoa elimu kwa wakulima na wafanyabiashara kuacha udanganyifu huo kwani unaathiri sekta nzima ya kilimo hicho nchini.
Alisema kuanzia msimu huu wa pamba utakaoanza Juni 27, mwaka huu, watatuma maofisa wao katika vituo vyote vinavyonunua pamba na kuhakikisha uuzaji unafanyika kwa kutumia vipimo sahihi kwa lengo la kumlinda mkulima na thamani ya pamba katika soko la dunia.

0 comments:
Post a Comment