Magufuli aahidi kushirikiana na wanasiasa*Apokea Ripoti ya Uchaguzi wa 2015 kutoka NEC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP mzee John Memose Cheyo mara baada ya kumaliza kuhutubia katika tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Fahmi Dovutwa mara baada ya kuhutubia katika tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mwanachama wa Chama cha UDP Goodluck Ole Medeye , Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo pamoja na Jaji Mark Bomani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Uchaguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Uchaguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Serikali, Tume ya Uchaguzi na Mabalozi wa nchi mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Uchaguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT baba Askofu Fredrick Shoo mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Uchaguzi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwanasiasa mkongwe John Shibuda huku Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein naye akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo mara baada ya kukamilika kwa tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Uchaguzi.
Na.Msaka Noti,Dar es Salaam
Rais wa Tanzania Dokta.John Pombe Magufuli amesema kuwa yupo pamoja na wanasiasa na atashirikiana nao vyema kwa kupokea ushauri, Maoni walio nayo kwa mikono miwili kwa kuwa ameamua kufanya kazi na vyama vyote vya siasa ili kuhakikisha kuwa anatatua kero zilizopo katika taifa na kuwataka kutambua kuwa uchaguzi ulishakwisha na sasa nivema kuiacha serikali ifanye kazi yake.
Amesema hayo wakati akikabidhiwa Ripoti ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka jana 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kuwa Uchaguzi umeisha na hakuna aliyeshinda wala aliyeshindwa watanzania wote wameshinda hivyo ni muda wa kuhakikisha nchi inasonga mbele.
Awali Kabla ya kumkabidhi Rais Ripoti ya Uchaguzi ya Mwaka jana 2015 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi NEC Jaji Damiani Lubuva alibainisha mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakiwakabili wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi kuwa ni kutokuwepo kwa jengo lake kwaajili ya shughuli hizo jambo lililofanya wawe wakipoteza fedha nyingi kulipia pango la ofisi hizo.
Kufuatia Changamoto hizo Rais Magufuli amelazimika kuzirudisha fedha ambazo alikabidhiwa na Tume hiyo kama kiasi kilicho baki wakati wa uchaguzi wa Mwaka 2015 na kuitaka Tume hiyo itumie fedha hizo Shilingi Bilioni 12 kwaajili ya kutengeneza Ofisi ya Jengo lake lenyewe.
Rais Magufuli amekiri wazi kwa Tume hiyo kuotokuwa na jengo lake na kusema kuwa itapendeza mno endapo NEC itazijenga ofisi hizo Mkoani Dodoma kama moja ya njia ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alisema Dodoma Makao Makuu ya Tanzania.
"Mimi mwenyewe nilishuhudia ukubwa wa changamoto hii ya kukosa jengo la ofisi hizi za tume (NEC) wakati nilipoenda kuchukua fomu za nakiri kwa dhati ofisi ya tume ilipo sio muafaka na ipo kwenye jengo la kupanga.
Pia ameipongeza tume ya Uchaguzi NEC kwa kusimamia vyema uchaguzi wa mwaka jana na kusema kuwa suala la uchaguzi ni tukio muhimu mno katika nchi kwani niwazi kuwa suala hilo huleta migogoro katika nchi, huku akitolea mfano baadhi ya nchi ambazo zimeingia kwenye migogoro na machafuko kutokana na masuala hayo ya uchaguzi na kukuta yakigharimu maisha ya wananchi wake.
Amekiri kuwa Uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa wenye ushindani mkali, na uliokuwa na mvuto wa kipekee ndani na nje ya nchi licha ya kuwa kwamba ni mara ya kwanza kutumia mfumo wa BVR katika mchakato huo.
Hata hivyo kwa upande wa Mwenyekiti wa NEC Jaji Damiani Lubuva ameongeza kwa kusema kuwa kama tume watahakikisha kuwa mapungufu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi uliopita watajitahidi kuyaboresha zaidi katika chaguzi ujao, nakusema kwamba NEC na ZEC zitaanza kushugulikia kura ya maoni,kuangalia sheria ya kura ya Maoni itakavyofanyiwa marekebisho hivyo kura ya maoni ipo pale pale kilicho badilika ni ratiba tu na NEC imeweza kuwa na daftari lake la kudumu na la kuaminika ambalo linaweza kutumika kwa chaguzi zijazo.
0 comments:
Post a Comment