Waziri mkuu Mhe Kassim Majaliwa amewatahadharisha watumishi wa ummawatakao husika na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo zitakazopelekwa katika ngazi ya wizara, taasisi na halmashauri baada ya kukamilika bunge la bajeti watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.
Akijibu maswali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema serikali itasimamia miradi inayotekelezwa kuwa na dhamani ya fedha inayoelekezwa katika eneo husika na kuhakikisha tija inapatikana.
Katika hatua nyingine serikali imewasilisha mswaada wa sheria ya fedha wa mwaka 2016 wenye lengo la kuwezesha utekelezaji wa kisheria wa bajeti ya serikali 2016/17 ambao unakusudia kufanya marekebisho sheria 16 zinazohusu fedha, kodi, ushuru, tozo na kuboresha ukusanyaji kodi.
Wakizungumza kuhusu mswaada huo baadhi ya wabunge wamekuwa wamesema ongezeko la kipengele katika mswaada huo kinachomtaka mnunuzi kuwa na risiti ya bidhaa ili aweze kukwepa mkono wa sheria wakati mashine ya kieletroniki za kulipa kodi haziko nchni nzima hususani maeneo ya vijijini.
Home
News
Slider
MAJALIWA:Tutawachukulia hatua watumishi wa umma watakaohusika na ubadhilifu wa fedha za Maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment