Image
Image

Makamu wa rais kuzindua jukwaa la uwezeshaji wanawake Kiuchumi.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es salaam siku ya Jumatatu, Juni 6, mwaka huu.
Uzinduzi wa jukwaa hilo utafanyika sambamba na uzinduzi wa Akaunti ya Malaika kwa ajili ya kuwafungulia akaunti wanawake wajasiriamali wadogo wa hapa nchini.  
Hafla hiyo inategemewa kuhudhuriwa na watu wapatao 1,000 kutoka makundi ya wadau mbalimbali wakiwemo wanawake wajasiriamali wa Tanzania Bara na Visiwani.
Jukwaa hilo litatoa uelewa kwa washiriki hususan kuhusu fursa zilizopo na mikakati ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali katika  harakati za kuinua wanawake kiuchumi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment