Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Anna Mghwira amesema kuna haja ya wanawake kujifunza mbinu za uongozi na kuchangamkia fursa za uongozi zilizopo kwenye ngazi mbalimbali ndani ya jamii ili kuepuka kutumiwa vibaya na wanasiasa.
Mghwira ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam kwenye kongamano lililoandaliwa na mtandao wa wanawake na katiba lililokuwa likirushwa na kituo cha ITV kujadili masuala mbalimbali ikiwemo nafasi za wabunge wa viti maalumu bungeni.
‘’Akinamama tujifunze mbinu za uongozi ,tujifunze kuielewa jamii yetu,kama hujaielewa basi hujaiva kwenye uongozi.Anna Mghwira.’’- Mghwira.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtandao wa kutetea wanawake katiba na uongozi Profesa Ruth Meena amesema kwamba wanawake ambao wana nafasi za uongozi katika vyama vya siasa watumie nafasi zao katika kubadilisha mifumo kandamizi na waonyeshe kweli mwanamke ana uwezo wa kuongoza.
Aidha wengi wa wachangiaji katika kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu ‘Mwanamke anaweza’ wamesema kwamba viti maalumu siyo tatizo kwani vipo kwa mujibu wa katiba na vinasaidia kuwasilisha hoja za msingi za wanawake kama afya ya uzazi na kutetea usawa wa kijinsia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment