Nguli
wa soka wa Argentina Diego Maradona amewataka mashabiki wa soka kuacha
kumsumbua Lionel Messi baada ya maamuzi yake ya kuamua kustaafu soka
katika timu ya taifa.
Messi ametangaza kustaafu soka baada ya timu ya
taifa ya Argentina kupoteza fainali ya tatu katika miaka mitatu baada
ya kufungwa na Chile 4-2 kwa mikwaju ya penalty katika mchezo wa fainali
ya Copa America Centenario.
Ilikuwa ni mara ya nne kwa Messi
kufungwa katika mchezo wa fainali katika mashindano makubwa, ikiwa ni
pamoja na mashindano ya mwaka 2007 na 2015 ya Copa, pamoja na fainali za
kombe la Dunia mwaka 2014 ambapo walifungwa fainali na Ujerumani.
Maamuzi
ya Messi yamewafanya mashabiki wengi wa Bara la Amerika Kusini kutokwa
na machozi ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa serikali
akiwemo raisi wa Argentina akimuomba Messi abatilishe maamuzi yake na
kurejea uwanjani kuitumikia timu ya taifa.
Hata hivyo Maradona ambaye
alishinda kombe la Dunia akiwa na Argentina mwaka 1986 amesisitiza kuwa
watu wanapaswa kumuacha Messi kwa wakati huu.
"Messi anatuambia kuacha kuusema mpira wake," Maradona.
"hii
ni sawa na Messi kutuambia kwamba anakwenda mapumziko, niacheni na
wakati mtakaponiita nitafikiria. Sitaki kulizungumzia hili zaidi'.
Anasema Maradona.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment