Polisi ya Uturuki imeendesha operesheni dhidi ya makundi yanayoshukiwa kuwa ya Dola la Kiislamu.
Polisi
ya Uturuki imeendesha operesheni dhidi ya makundi yanayoshukiwa kuwa ya
Dola la Kiislamu mjini Istanbul na mji wa pwani ya bahari ya Aegean wa
Izmir, siku mbili baada ya mashambulizi matatu ya kujitoa muhanga
yaliyouwa watu 42 katika uwanja wa ndege wa Istanbul. Polisi wa
kupambana na ugaidi wakiongozwa na vikosi maalumu wamefanya uvamizi
katika maeneo matatu yanayokaliwa na wafanyakazi mjini Istanbul -
limesema shirika la habari la serikali Anadolu bila kutaja vyanzo vyake.
Wakati huo washukiwa tisa wanaodhaniwa kuwasiliana na wanachama wa
kundi la IS nchini Syria, walikamatwa katika uvamizi katika wilaya tatu
za Izmir, wakituhumiwa kwa kufadhili, kuandikisha na kutoa msaada wa
usafiri kwa kundi hilo la itikadi kali. Awali vikosi vya usalama
vimeripotiwa kuwauwa washukiwa wawili wa Dola la Kiislamu kwenye mpaka
wa Syria, ambao inaamiwa walikuwa wanapanga njama ya kufanya
mashambulizi ya kujitoa muhanga nchini Uturuki.
0 comments:
Post a Comment