Kansela
Angela Merkel wa Ujerumani ameionya Uingereza isitarajia kuendelea
kupata faida ilizokuwa ikizipata katika Umoja wa Ulaya, hata baada ya
kuamua kujitenga na Umoja huo.
Akizungumza katika mkutano maalum
mjini Berlin kabla ya kwenda Brussels kushiriki katika mkutano wa wakuu
wa Umoja wa Ulaya, Bi Merkel amesema ukijiondoa katika familia, huwezi
kuendelea kunufaika bila kuwajibika.
Merkel amesisitiza kuwa
hayatakuwepo mazungumzo yoyote na Uingereza, yawe rasmi au vinginevyo,
kabla ya nchi hiyo kuwasilisha ombi la kujiondoa katika Umoja huo.
Bi
Merkel amesema kujiondoa kwa Uingereza, maarufu kama Brexit, hakuwezi
kuipotosha Ulaya katika kushughulikia changamoto kubwa zilizopo. Mkutano
wa Brussels unajadili hatua ya Uingereza kuondoa uanachama wake katika
Umoja wa Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment