Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha makusanyo ya mapato na kudhibiti upotevu wa fedha katika vyanzo mbalimbali ili kuhakikisha fedha zinapelekwa Hazina kama ilivyopangwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika mwaka ujao wa fedha 2016/17.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI- Mheshimiwa SELEMANI JAFO wakati akijibu swali Bungeni ambapo kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi ISACK KAMWELWE alisema katika mwaka ujao wa fedha Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni mia 992.8 kwa ajili ya miradi ya maji katika halmashauri ya mji wa Makambako Mkoani Njombe.
Naye Naibu wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto DR. HAMISI KIGWANGALA kwa niaba ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga ameliambia Bunge kwamba serikali haina mpango wa kuzishawishi nchi zilizopata hifadhi ya wapigania uhuru hapa nchni kusaidia juhudi za uhifadhi wa kumbukumbu katika maeneo waliokuwa wakiishi.
Wakati huo Serikali imesema hakuna kodi inayotozwa kwa nia ya kuua mitaji ya wafanyabiashara kutokana kutoza kiwango cha juu kodi ya mapato ya asilimia 30 ya mapato baada ya kuondoa gharama za biashara.
Akijibu swali bungeni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango DR. ASHATU KIJAJI amesema mfanyabiashara asipopata faida hakuna kodi ya mapato itakayotozwa hivyo kodi zinazotozwa na mamlaka ya mapato nchni-TRA- ni halali na haziui mitaji ya wafanyabiashara wetu.
Home
News
Slider
Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha makusanyo ya mapato na kudhibiti upotevu wa fedha.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment