Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango, amewataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari ili kuiwezesha serikali kutekeleza kwa vitendo Bajeti Kuu ya serikali iliyopitishwa kwa kishindo hapo jana.
Dokta Mpango ametoa wito huo katika viunga vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mara baada ya wabunge kupitisha bajeti hiyo kwa asilimia 100
Waziri huyo wa fedha na Mipango ameanza kwa kueleza namna ambavyo serikali inatarajia kutekeleza bajeti hiyo
Amesema kuwa ili kufikia malengo hayo wadau wanatakiwa kuiunga mkono serikali kwa kulipa kodi huku akiahidi kuziba mianya ya matumizi mabaya ya fedha za serikali
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha amesema kuwa Bajeti iliyopitishwa itatekelezwa kwa viwango
Baadhi ya Wabunge wamesema kuwa Bajeti iliyopitishwa inaleta matumaini katika kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka kwa kuimarisha viwanda na kukuza ahira
Jana Bunge limepitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya serikali yenye malengo ya kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Triln 29.54, ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zitatumika kwaajili ya miradi ya maendeleo na kiasi kilichobaki kitatumika kwa matumizi ya kawaida.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment