Akijibu
swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyetaka kujua
hatua ambayo serikali inachukua baada ya kubainika kuwa kuna wanasiasa
wanahamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, Waziri wa Mambo ya Ndani,
Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa Serikali haitavumilia kuona mtu ama
kundi lolote likihatarisha amani na utulivu wa nchi kwa njia yoyote ile.
Amesema kuwa kuna tabia imeanza kujitokeza kwa baadhi ya wanasiasa hasa
wa vyama vya upinzani kutoa matamshi yenye kuchochea vurugu, uvunjifu
wa amani na hata umwagaji damu. Amesema kuwa wizara yake kupitia Jeshi
la Polisi itahakikisha kuwa vitendo hivyo vinakomeshwa mara moja ili
nchi iemdeleee kuwa ya amani
" Mheshimiwa Naibu Spika, nimewaagiza
vijana wangu ( polisi) kuwashughulikia wale tu vinara na si kuhangaika
na wananchi wasio na hatia ambao wanapelekeshwa tu na wanasiasa hao.
Amesema kuwa ipo tabia ya baadhi ya wanasiasa kutoa maneno ya uchochezi
na kuwatanguliza wananchi wasio na hatia na pindi jeshi la polisi
linapochukua hatua, wanaoathirika ni wananchi hao na si wale
waliochochea. Kwa hali hiyo jeshi la polisi limeshabadili mbinu za
kupambana na vitendo hivyo na badala yake itashugulika na wale vinara
tu" Aliongeza Waziri.
Mytake: Niwapongeze Jeshi la Polisi na Wizara
ya Mambo ya ndani kwa kuliona hili. Hii ndio njia muafaka ya kuwatulia
hawa wahalifu bila ya kuleta madhara. Naona kazi imeshaanza hasa kwa
kuwaita na kuwahoji baadhi ya wanasiasa wa upinzani akiwemo Mbowe, Tundu
Lissu, Zitto Kabwe, Ole Sosopi, Kubenea nk. Kazi imeshaanza. Heshima
inarudi.
sOURCE:JF.
Home
News
Slider
Mwigulu Nchemba: Nimewaelekeza polisi kuwashughulikia vinara wa vurugu na uchochezi
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment