Image
Image

Ndege iliyoanguka ya Misiri yaripotiwa kutua kwa dharura mara tatu ndani ya saa 24 kabla ya ajali

Ndege ya shirika la ndege la Misri EgyptAir iliyoanguka Mei 19 iliripotiwa kutua kwa dharura kwa takriban mara tatu ndani ya saa 24 kabla ya kukumbwa na ajali ya mwisho.
Televisheni ya Ufaransa, France 3, imesema kabla ya kwenda Cairo kutoka Paris, ndege hiyo ilifanya safari nyingi kati ya Mei 18 na 19. Katika kipindi hicho, mfumo wa tahadhari wa ndege ulionesha hali isiyo ya kawaida baada ya kuruka kutoka Asmara, Cairo na Tunisia, alama ambayo iliilazimisha ndege hiyo kurudi na kufanyiwa ukaguzi wa kiufundi.
Ripoti hiyo inasema, takwimu hizo za kiufundi zinatokana na ripoti ya mfumo wa mawasliano wa ndege hiyo.
Wakati huohuo, habari zinasema meli ya jeshi la majini la Ufaransa inayoshiriki kutafuta mabaki ya ndege hiyo huenda ilipata alama kutoka kwa sanduku nyeusi la ndege hiyo iliyoanguka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment