Wakulima na wanunuzi wa zao la pamba katika mikoa ya kanda ya Mangaribi wamehimizwa kuzingatia ubora wa zao na usafi wa zao hilo ili liweze kupata soko la uhakika.
Akitoa ombi hilo, mkaguzi wa viwanda vya pamba Kisinza Ndimu amesema wakulima na wanunuzi wa zao hilo wamekuwa wakiharibu kwa makusudi ubora na usafi wa zao la pamba, hali ambayo imekuwa ikisababisha thamani yake kushuka kila mwaka.
Alisema wanunuzi wamekuwa wakifanya uharibifu huo kwa asilimia zaidi ya 80 wakati inapofika katika vituo vyao vya kununulia pamba na akayataka makundi yote mawili, pamoja na wadau mbalimbali kuzingatia ubora na usafi wa zao hilo.
Hata jivyo baadhi ya wanunuzi wa zao hilo pamoja na wakulima wamesema kuna changamoto nyingi zinazowakabili wakulima, ikiwemo kutopata pembejeo kwa wakati, pamoja na kupewa dawa za kuua wadudu ambazo hazina uwezo, pamoja na mbegu ambazo hazioti.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment