Ndege ya shirika la ndege la EgyptAir ililazimika kutua kwa dharura nchini Uzbekistan baada ya kuwa na tishio la bomu.
Abiria 118 na wafanyakazi 17 waliokuwa katika ndege hiyo aina ya A330-220 walilazimika kushuka kutoka kwa ndege hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa Urgench .
Hata hivyo maafisa wa Misri walisema kuwa vikosi vya usalama vya Uzbek walifanya uchunguzi kwa kutafuta tafuta lakini hamna kilipuzi chochote kilichopatikana.
Wiki tatu zilizopita ndege moja ya shirika la EgyptAir iliyokuwa imebeba watu 66 ilipotea katika bahari ya Mediterania.
Chanzo cha ajali hiyo bado ni kitendawili ingawaje maafisa wa Misri ni kitendo cha kigaidi na wala si hitilafu za kiufundi.
Juma lililopita wachunguzi wa kifaransa walifahammisha kuwa na visanduku vyeusi vilivyogundulika kutoka kilomita 290 kaskazini mwa pwani ya Misri.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment