Image
Image

Nyanda amejitoa kushiriki uchaguzi Yanga.

MGOMBEA wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, ambaye alichukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Aaron Nyanda amejitoa kushiriki uchaguzi huo kwa madai muda wa kufanya kampeni ni mfupi.
Akizungumza jana, Nyanda alisema ameamua kujitoa kwa sababu muda uliobaki kufanya kampeni ni mfupi, kwani uchaguzi umepangwa kufanyika kesho. “Nimeamua kujitoa kwa vile muda ni mchache tofauti na mchakato ule ambao TFF waliutangaza awali, huku ukiangalia muda umeisha kesho (leo) mwisho wa kampeni, sasa utafanyaje kampeni ya siku moja bila kujipanga, ndio maana nimeamua kukaa pembeni nipishe msongamano,” alisema Nyanda mchezaji wa zamani wa Yanga na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.
Akizungumza kuhusiana na suala hilo Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Bakili Makele alisema wagombea waliojitoa ambao walichukua fomu TFF wamerudishiwa fedha zao, huku wale waliotaka kuendelea na mchakato wa uchaguzi wakilazimika kujaza fomu upya na kufanyiwa usaili jana mchana.
Lakini wakati Nyanda akijitoa, mgombea mwingine wa nafasi hiyo aliyekuwa amechukua fomu TFF, Tito Osoro alisema yeye atapambana hadi dakika ya mwisho. Tito alifanyiwa usaili na baadae aliruhusiwa kuendelea na kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo.
Wagombea wengine waliochukua fomu TFF walifanyiwa usaili jana na kuruhusiwa kuanza kampeni jana hiyohiyo, ambao ni Edgar Chibura, Ramadhan Kampira, Paschal Laizer na Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’.
Wagombea Said Omary na Mchafu Chakoma walikuwa hawajafika kwenye ofisi hizo, kuchukua ama fomu ili waendelee na uchaguzi au kujitoa na kurudishiwa fedha zao. Awali uchaguzi huo wa Yanga ulipangwa kufanyika Juni 25 ukisimamiwa na TFF, hata hivyo ulizuka mvutano mkubwa kwa Yanga kugoma kusimamiwa uchaguzi wake na TFF.
Wakati TFF ikiendelea na mchakato wa utoaji wa fomu za Yanga, uongozi wa klabu hiyo nao ulitangaza mchakato wake na kupanga uchaguzi ufanyike kesho. Kufuatia mvutano huo, juzi TFF ilikutana na viongozi wa Yanga na kufikia uamuzi wa kuiruhusu Yanga ifanye uchaguzi kwa kujisimamia yenyewe.
Hata hivyo kikao hicho kilikubaliana wagombea waliochukua fomu TFF wahusishwe katika mchakato huo kama walivyo wagombea wengine 19 waliochukua fomu makao makuu ya Yanga.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment