Rais wa Marekani Barack Obama ameshutumu matamshi ya Donald Trump kufuatia mashambulizi ya kinyama ya risasi ambapo watu 49 waliuwawa katika klabu ya mashoga jimboni Florida mwishoni mwa juma.
Trump ambaye anaelekea kupata uteuzi kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican, alitumia mashambulizi hayo kuongeza kasi katika matamshi yake dhidi ya Uislamu, akirudia miito yake ya kutaka kupigwa marufuku kwa muda Waislamu kuingia nchini Marekani.
Katika hotuba, Obama alimweleza Trump kuwa ni kitisho kwa usalama wa taifa.
Matamshi ya rais Obama yanafuatia ukosoaji ulitolewa na Trump dhidi yake , ambae alisema Obama analazimika kujiuzulu kwasababu amekataa kuyaeleza mashambulio ya Orlando kuwa ni tukio la Uislamu wa itikadi kali.
Wakati huo huo mke wa mshambuliaji huyo wa Orlando, Omar Mateen, anaweza kushitakiwa kuwa ni mshirika wa shambulio hilo, kwasababu huenda alifahamu kwamba mume wake anapanga mashambulizi.
Jopo la washauri wa mahakama limeundwa na linaweza kuanza kazi kuanzia mapema leo.
Home
Kimataifa
Slider
Obama ashutumu matamshi ya Donald Trump dhidi ya mauaji ya wapenzi wa jinsia moja.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment