Image
Image

Serikali kuziwezesha Hospitali za rufaa za mikoa zinatoa huduma ya Matibabu ya Fistula.

Serikali imesema inafanya jitihada kuziwezesha hospitali  za  Rufaa  za mikoa zinatoa huduma za matibabu  ya  Fistula.
Hayo yamesemwa na Waziri wa  Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee   na  Watoto , UMMY MWALIMU alipokuwa kijibu swali la  Mbunge wa Viti Maalum,MGENI JADI KADIG A  aliyetaka kuju a  serikali ina mapango gani  wa kutokomeza tatizo la  ugonjwa wa Fistula nchini.
Ameliambia bunge kuwa  tatizo la fistula  linatokana na   mjamzito   kupata uchungu pingamizi  kwa muda  mrefu  na kwamba   tatizo  hilo  linaweza  kuepukwa  kwa  kuboresha  huduma  kwa  wajawazito .
Amesema ili kuboresha  huduma kwa wajawazito  wizara  imekuwa inatekeleza   hatua   mbalimbali kama   kuelimisha jamii kupitia  huduma  za afya  katika jamii  na vyombo  vya habari kuhusu umuhimu wa kujifungulia  katika vituo  vya kutolea  huduma  ya afya.
Like ukurasa wetu wa Facebook hapo, kwa kuweza kupata taarifa zaidi, kila zinapo tufikia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment