Hospitali teule ya Mugana iliyoko wilayani Misenyi mkoani Kagera kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali za Izaas lililoko mkoani humo inatarajia kutoa bure huduma ya upasuaji mkubwa zaidi kwa watu 150 wenye huitaji wanaokabiliwa na magonjwa ya aina mbalimbali ambayo ni pamoja na tezi la shingo.
mganga mfawidhi wa hospitali ya Mugana, Dkt. Johakim Mazima amesema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la upasuaji uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Salum Mstapha Kijuu amefanya uzinduzi huo kwa kuwashuhudia baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakipasuliwa kwenye chumba cha upasuaji cha hospitali hiyo.
Kwa upande wake, mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerarli Salum Mstapha Kijuu ameahidi kuwa serikali ya mkoa wa Kagera itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wanajitokeza kwa lengo la kuimarisha afya ndani ya jamii, naye mratibu wa shirika la Izaas, Fazal Raza ameelezea sababu za kuwasaidi wenye huitaji na ameiomba jamii iache vitendo vya kuwanyanyapaa walemavu, huku baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakisumbuliwa na tezi la shingo wakieleza hali zao kwa sasa baada kufanyiwa upasuaji.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment