Image
Image

Yanga inakibarua kizito kusaka point 3 kwa wababe mara 5 Afrika TP Mazembe.

WAWAKILISHI pekee katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga leo watakuwa na kazi nzito ya kusaka pointi tatu mbele ya mabingwa mara tano wa Afrika, TP Mazembe ya Congo DR, katika mchezo wa hatua ya makundi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya MO Bejaia ya Algeria kwa kufungwa bao 1-0 na kujikuta ikishika nafasi ya tatu kwenye kundi A huku wapinzani wao hao wakiongoza kundi hilo baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-1 dhidi ya Medeama ya Ghana.
Kitendo cha kupoteza mchezo wa kwanza ugenini, kitawapa presha na hasira Yanga kucheza kwa juhudi kwenye uwanja wake wa nyumbani ili kupata ushindi dhidi ya Mazembe.
Wakati leo wakiwa kibaruani, huenda wakawakosa nyota watatu ambao ni Simon Msuva anayeugua malaria, Amissi Tambwe na beki Haji Mwinyi wanaotumikia adhabu ya kadi. Katika kuhakikisha mchezo huo wanafanya vizuri waliweka kambi nchini Uturuki na kurejea Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, wakiwa na imani ya kufanya vizuri.
Matarajio ya wengi katika kikosi hicho ni kumuona nyota mpya aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, Obrey Chirwa.
Pia, nyota waliokosa mchezo uliopita kwa majeraha na kadi Juma Abdul na nahodha Nadir Haroub ‘Canavaro’ wanatarajiwa kuwepo leo, kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe.
Yanga inakutana na timu ambayo ina uwezo mkubwa katika michuano ya kimataifa hivyo, wa nahitaji kucheza kwa tahadhari na kupata ushindi wa mapema.
Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm, alisema anajua kuwa TP Mazembe ni timu bora Afrika, hivyo, wamejipanga kupambana nao ili kupata ushindi.
“Lengo letu ni kupata pointi tatu, nimezungumza na wachezaji na kuwajenga kisaikolojia kucheza kwa kutulia kwa ajili ya kupata matokeo,” alisema.
Mechi hiyo inatarajiwa kushuhudiwa na tajiri wa mmiliki wa Mazembe, Moise Katumbi. Mchezaji anayeogopwa katika kikosi hicho ni Ranfled Kalaba aliyefunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Medeama hivi karibuni.
Pia, Mtanzania Thomas Ulimwengu ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ili kutoa hamasa zaidi kwa wachezaji, mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ametoa ofa na sasa mashabiki wataingia bure uwanjani kushuhudia mechi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment