Baraza la usalama la UN limetangaza kuongeza muda wa kuhudumu kwa kikosi cha kulinda amani cha AMISOM nchini Somalia hadi tarehe 31 Mei 2017.
Baraza
hilo lilitoa maelezo hapo jana siku Alhamisi na kuarifu kuchukuwa
uamuzi huo kutokana na vitisho vya Al-Shabaab vilivyoongezeka katika
kanda hiyo.
Vile vile, baraza la usalama la UN pia litahakikisha
idadi ya wanajeshi wa AMISOM itafikia 22,126 wanaojumuisha askari kutoka
mataifa 15.
UN pia imeanzisha mpango maalum wa AMISOM ambapo wanajeshi watatarajiwa kuelimisha jamii kuhusiana na umuhimu wa usalama hasa katika maeneo yaliyokombolewa kutoka mikononi mwa Al-Shabaab.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment